Radio Ebony FM yenye
makao yake makuu mkoani Iringa na inayorusha matangazo yake katika masafa
ya 87.8 (Iringa), 88.2 (Makambako), 94.7 (Mbeya), 91.6 (Dodoma), 95.4
(Morogoro) na 102.2 (Songea) jana Oct 01 kupitia kipindi chake cha mchana
"THE SPLASH" imezindua hewani (on air launching) TAMASHA lake kubwa
la kila mwaka maarufu kwa jina la "MTIKISIKO" ambalo linatarajiwa
kuanza katikati ya mwezi huu na kupita karibu sehemu zote inaposikika redio
hiyo.
Dj Alikoko (Manager Ebony Ent)
Akizungumza katika uzinduzi huo Promotions Manager wa EBONY FM Bonny Zacharia Nyatogo amesema, mwaka huu EBONY FM ikishirikiana na kampuni mama ya burudani EBONY ENTERTAINMENT wamejipanga vya kutosha kukata kiu ya burudani kwa wapenda burudani wote kwenye mikoa ya Nyanda Za Juu Kusini ambayo wana uhakika haijakatwa bado.
Promotions Manager Bonnsly akijiandaa kuzungungumza
Promotions Manager Bonny Zacharia Nyatogo
Mratibu mkuu ni Eddo Bashir kama ilivyo kwa miaka iliyopita, naye amesema maandilizi ya TAMASHA hilo yameshaanza na muda wowote kuanzia sasa ratiba rasmi itatangazwa hasa tarehe na maeneo TAMASHA hilo litakapopita. Kauli mbiu ya TAMASHA hilo mwaka huu ni "Ndo Vileee..!!!"
Shangweeeeee
Launching continues
"The Splash host"...Mkazuzu
Tamasha la "MTIKISIKO" kihistoria lilianza mwaka 2007 wakati huo
likiitwa "PAMOJA TIME" ambapo mwaka 2008 lilibadilishwa jina na
kuanza rasmi kuitwa "MTIKISIKO"...nia na madhumuni ya TAMASHA la
"MTIKISIKO" ni kukutana pamoja na wasikilizaji wa ukweli wa EBONY FM
na kurudisha kwao LOVE wanayotoa kwa redio.
0 comments:
Post a Comment